Homa Bay County Pundit

MKE BADO

Sitaoa mimi, sababu zangu ni za kibinafsi,
Ndoa itanifunga, nitakuwa kwenye jela,
Mke akiwa polisi, anilinde nyumbani,
Bado nangoja naogopa kuoa.

Akiniona na yule, mke wa jirani mara mbili tatu,
Faraghani tukizungumza, mambo ya kawaida tu,
Atanishuku aniulize, katu langu jibu hatakubali anisomee,
Bado nangoja naogopa kuoa

Nikimchosha weye, hatasita asilani,
Mahakamani kunipeleka, kunishtaki kutofanya wangu wajibu,
Hakimu akimsikiliza, kifungu nitapewa nakwambia,
Bado nangoja naogopa kuoa.

Hukumbuki yule rafiki, alizirai siku kuu,
Bibi harusi katoroka, na bwana mwengine tofauti,
Maajabu hayo jameni, aibu za mke naogopa mie,
Bado nangoja naogopa kuoa.

Kelele zake ja kasuku, jikoni nikikosa kumsaidia,
Eti sote sawa atasema, hata nguo zetu nifue nianike,
Nikikataa eti mi si mume, ampigia yule wa kando,
Bado nangoja naogopa kuoa.

Kisha talaka nimpe, mali yetu adai tugawe bila shaka,
Anishushe hadhi jamiini, wazazi wakose imani nami,
Baraza la wazee pia wao, kesi kutofuata mila desturi,
Bado nangoja naogopa kuoa.

image

Photo: courtesy.

Limetungwa Na Mwalimu Emmanuel Odira

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this:
close-alt close collapse comment ellipsis expand gallery heart lock menu next pinned previous reply search share star