Homa Bay County Pundit

MWALIMU HAKULIPWA

Uliponiajiri wewe, malipo bora kuniahidi,
Ulifikiria nini, hadi sasa umenigeuka,
Unajifanya hunijui, wewe maji mie mafuta,
Mimi Mwalimu, Mnyonge kilio changu atasikia nani?

Sasa umekuwa kama nguva, yule wa baharini,
Kichwa chake binadamu, kiwiliwili samaki,
Yaani ukidhani ni mrembo, ngoja hutaona miguu,
Mimi Mwalimu, Maskini sina haki.

Uliponiajiri wewe, Ulisema unafahamu yangu kazi,
Hakuna tofauti na yule, wa jua kali na sulubu,
Mimi mmoja darasani, wanafunzi mia kuningoja,
Mimi Mwalimu, Mnyonge kilio changu atasikia nani?

Sasa umekuwa kama popo, yule hutatanisha,
Ukisema ni ndege, kweli hu’ruka,
Yule asema ni mnyama, hajakosea ni mamalia,
Mimi Mwalimu, maskini sina haki.

Uliponiajiri wewe, tulikubaliana kwa ufasaha,
Sahihi nikatia, kuwa wewe mwajiri utanitunza,
Sasa wataka kandarasi, uweze kunifuta utakapo,
Mimi Mwalimu, Mnyonge kilio changu atasikia nani?

Sasa umekuwa kama kinyonga, yule anayebadilika,
Huchukua rangi ile, ya mazingira alipo,
Yaani ukidhani yupo, hataonekana utashangaa,
Mimi Mwalimu, Maskini sina haki.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this:
close-alt close collapse comment ellipsis expand gallery heart lock menu next pinned previous reply search share star